UNAWEZA KUTEMBEA UMBALI KIASI GANI UKIWA PEKU? Mwandishi wa “Safari ya Juma” anakualika uifuatilie simulizi ya kijana Juma aliyetembea peku umbali wa kilomita 1529 kutoka Mbeya iliyopo kusini hadi Arusha iliyopo kaskazini mwa Tanzania. Masaa kadhaa kabla ya kufariki, Juma alimwahidi mamake kuwa angemtafuta mzungu mmishenari aliyeko Mbeya ili amweleze habari za Yesu. Juma agundua kua yule mzungu ameishaondoka Mbeya kuelekea Arusha na hivyo hana budi kumfuata huko ili kuitunza ahadi aliyomwahidi mama yake ambaye sasa ni marehemu. Katika safari hii hatari, Juma akumbana na vipingamizi vingi vya kimwili na kiroho pia. Utamhurumia anapokumbana na chui na kulengwa na majangili, anapotekwa na kutumikishwa kiutumwa. Je! atasalimika kutoka katika mikono ya mbwa-mwitu wakali wanaomwinda msituni? Akiwa amepoteza fahamu na ni mgonjwa amelala kando ya barabara, Je! kuna matumaini yeyote ya kuokolewa? Je, atafika Arusha? Soma kitabu hiki ili kupata majibu!
"synopsis" may belong to another edition of this title.
Baada ya kutumika kwa miaka 23 katika sekta ya sayansi ya teknolojia (Miaka 16 na Texas Instruments), Edwin Scroggins aliamua kubadili fani yake. Ili kujiandaa katika sekta ya elimu ya Kikristo, Edwin alijiunga na chuo na kupokea shahada ya Elimu ya Biblia na pia kupokea Shahada ya juu ya elimu ya watu wazima. Mwaka 1978, Edwin alijiunga na chuo cha Dallas Bible College kama mmojawapo wa wakufunzi. Alitumika katika chuo hicho kama msaaidizi wa raisi wa chuo katika kuandika miradi mbalimbali ili kupata misaada kutoka katika taasisi tofauti tofauti, pia alikuwa mkufunzi hapo chuoni na mratibu wa mitaala mbalimbali kwa wanafunzi walioko nje ya chuo. Miongoni mwa vitabu alivyoandika ni pamoja na Prophecy for Today kilichochapwa na Chuo cha Biblia cha Dallas mwaka 1971, na pia kitabu kiitwacho Bible Prophecy in a nutshell, kilichochapwa na BookSurge mwaka 2007. Aidha vitabu vingine kama, Strawberry Lane na Return to Strawberry Lane, vyote vilichapwa na BookSurge mwaka 2007. Kitabu kiingine kiitwacho How I Built My Retreat Cabin in the Woods and Lived to Write About It kilichapwa na BookSurge mwaka 2008. Mwaka 2010, kampuni ya CreateSpace Ilichapa kitabu kingine cha Edwin kiitwacho The Promise and Passion of Christ the King. Toka mwaka 1961, Edwin amekuwa akiishi katika mji wa Richardson, Texas pamoja na mkewe Alma, ambaye wameishi pamoja kwa miaka 61. Mke wake alifariki Aprili, 2011, na Edwin alikusanya kila kitu ambacho mke wake alikuwa akiandika na kisha kuandika kitabu kiitwacho Songs in the Night: Memories of Alma Grace Scroggins (Kilichapwa na CreateSpace mwaka 2012). Edwin anaendelea kuishi katika nyumba yake ambayo yeye na mke wake wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka 50.
"About this title" may belong to another edition of this title.
Seller: GreatBookPrices, Columbia, MD, U.S.A.
Condition: As New. Unread book in perfect condition. Seller Inventory # 21481405
Seller: California Books, Miami, FL, U.S.A.
Condition: New. Print on Demand. Seller Inventory # I-9781499359862
Seller: GreatBookPrices, Columbia, MD, U.S.A.
Condition: New. Seller Inventory # 21481405-n
Seller: THE SAINT BOOKSTORE, Southport, United Kingdom
Paperback / softback. Condition: New. This item is printed on demand. New copy - Usually dispatched within 5-9 working days. Seller Inventory # C9781499359862
Quantity: Over 20 available
Seller: GreatBookPricesUK, Woodford Green, United Kingdom
Condition: As New. Unread book in perfect condition. Seller Inventory # 21481405
Quantity: Over 20 available
Seller: GreatBookPricesUK, Woodford Green, United Kingdom
Condition: New. Seller Inventory # 21481405-n
Quantity: Over 20 available
Seller: CitiRetail, Stevenage, United Kingdom
Paperback. Condition: new. Paperback. UNAWEZA KUTEMBEA UMBALI KIASI GANI UKIWA PEKU? Mwandishi wa "Safari ya Juma" anakualika uifuatilie simulizi ya kijana Juma aliyetembea peku umbali wa kilomita 1529 kutoka Mbeya iliyopo kusini hadi Arusha iliyopo kaskazini mwa Tanzania. Masaa kadhaa kabla ya kufariki, Juma alimwahidi mamake kuwa angemtafuta mzungu mmishenari aliyeko Mbeya ili amweleze habari za Yesu. Juma agundua kua yule mzungu ameishaondoka Mbeya kuelekea Arusha na hivyo hana budi kumfuata huko ili kuitunza ahadi aliyomwahidi mama yake ambaye sasa ni marehemu. Katika safari hii hatari, Juma akumbana na vipingamizi vingi vya kimwili na kiroho pia. Utamhurumia anapokumbana na chui na kulengwa na majangili, anapotekwa na kutumikishwa kiutumwa. Je! atasalimika kutoka katika mikono ya mbwa-mwitu wakali wanaomwinda msituni? Akiwa amepoteza fahamu na ni mgonjwa amelala kando ya barabara, Je! kuna matumaini yeyote ya kuokolewa? Je, atafika Arusha? Soma kitabu hiki ili kupata majibu! This item is printed on demand. Shipping may be from our UK warehouse or from our Australian or US warehouses, depending on stock availability. Seller Inventory # 9781499359862
Quantity: 1 available